Makubaliano yanayofuata ya Leseni ya Mtumiaji wa Mwisho (“EULA”) yanahusu makubaliano kati ya KAI OS TECHNOLOGIES (HONG KONG) LIMITED, ikiwa ni pamoja na washiriki wake (“sisi” au “KAI”) na wewe, na unadhibiti matumizi yako ya Programu na Huduma. Tafadhali soma EULA hii kwa makini. Tafadhali kumbuka kwamba lazima uwe na haki ya kisheria kuingia kwenye makubaliano ya hali hii ili uweze kutumia Programu na Huduma.

Unakubali EULA hii kwa kutumia programu inayoitwa “KaiOS”, ikiwa ni pamoja na usasisho, maboresho, vijenzi vyovyote vya ziada vilivyoshirikishwa,programu yoyote (ikiwa ni pamoja na programu kupitia wavuti), programu-tumizi, maudhui au Huduma za KAI zinazotolewa kulingana na EULA hii, na hati zote za programu (“Programu”).

 

Kumbuka kwamba baadhi ya vijenzi vya Programu yetu vinapatikana kama chanzo huriakupitia miradi mbalimbali (“Programu ya Chanzo Huria”). Ingawa Programu iko chini ya EULA hii, Programu ya Chanzo Huria inapatikana kulingana na masharti yake, ambayo unaweza kuitumia kulingana na masharti yake.

 

Zaidi ya Programu ya Chanzo Huria, Programu hii inaweza kujumuisha programu zingine za washirika wa tatu chini ya leseni tofauti (ambazo, pamoja na Proramu ya Chanzo Huria zinajulikana kama “Programu za Washirika wa Tatu”). Programu hizi za Washirika wa Tatu zinawea kuwa chini ya masharti ya leseni tofauti ambayo lazima uyakubali ili uweze kuzitumia.

 

Kwa kukubali EULA hii au kwa kuitumia Programu na/au Huduma, unakubali masharti haya yote, na unakubali usambazaji wa taarifa fulani wakati wa uamilishaji na wakati wa unaitumia kulingana na Fungu 2.

 1. UPEO WA LESENI

Programu hii na maudhui yote yanayofikiwa kupitia Programu yanapeanwa kwa leseni, hayauzwi. Kwa kuzingatia mapatano yako, EULA hii inakupatia tu haki za kutumia na kuendesha Programu hii mara moja kwenye kifaa chako ambapo Programu hii ilisakinishwa kabla. Huwezi kuisambazaau kuipeana Programu hii kupitia mtandao ambapo inaweza kutumiwa na vifaa vingi kwa wakati mmoja. KAI, wagawaji wake na washiriki waliopewa leseni wanahifadhi haki zote zingine. Isipokuwa ishurutishwe vinginevyo na sheria husika au masharti ya leseni ya Programu ya Washirika wa Tatu, unaweza kutumia Programu hii inavyoruhusiwa katika EULA peke yake. Kwa kufanya hivyo, lazima utii vikwazo vyovyote vya kiufundi katika Programu vinavyokuruhusu kuitumia kwa namna fulani tu. Huruhusiwi:

 • kunakili, kusambaza, kubadilisha au kuchapisha Programu hii;
 • kuruka ukaguzi wowote wa uhalalishaji au vikwazo vya kiufundi katika Programu hii;
 • kutumia Programu hii kwa madhumuni yoyote kinyume na sheria, laghai au yasiyoidhinishwa;
 • kusambaza virusi vyovyote, au msimbo wowote haribifu;
 • kutupatia taarifa isiyo ya kweli au ya kupotosha;
 • kukusanya data yoyote ya kibinafsi au taarifa yoyote inayoweza kutambulisha mtu binafsi ya washiriki wa tatu kinyume na ulinzi wowote wa data na/au sheria za faragha;
 • kuhandisi-kinyume au kutenganisha Programu hii, isipokuwa na kwa kiwango kinachoruhusiwa sheria huska peke yake, licha ya vikwazo vyake; au
 • kuhamisha Programu hii au EULA hii kwa mshiriki yoyote wa tatu isipokuwa ni pamoja na kifaa chenye Programu hii.

Ikiwa sisi, kwa hiari yetu busara, tutazingatia kwamba unakiuka sheria zozote, sheria za leseni au EULA hii, tuna haki ya, zaidi ya masuluhisho mengine yanayopatikana, kusimamisha ufikiaji wako kwa Programu na Huduma.

 1. FARAGHA; KIBALI CHA KUTUMIA DATA

Baadhi ya Programu na Huduma zinaweza kutuma au kupokea taarifa wakati unaziamilisha au kuzitumia. Kwa kukubali EULA hii na kutumia Programu hii na/au Huduma hizi unakubali kwamba tunaweza kukusanya, kutumia, na kufichua taarifa kama ilivyofafanuliwa katika Sera ya Faragha ya KaiOS.

 1. VIKWAZO VYA UHAMISHAJI

Programu hii huenda ikawa chini ya sheria na kanuni zinazodhibiti uhamishaji za Marekani au nchi zingine zinazoweza kuzuia au kupiga marufuku uhamishaji wa nje ya nchi, uhamishaji upya wa nje ya nchi au uhamishaji wa Programu hii. Lazima utii sheria na kanuni zote zinazotumika zinazodhibiti uhamishaji wa nje ya nchi na uhamishaji upya wa nje ya nchi. Kwa taarifa au maulizo zaidi, tafadhali wasiliana na huduma zetu kwa wateja.

 1. MAKUBALIANO KAMILI

EULA hii, Sera ya Faragha ya KaiOS na masharti yanayoambatana na usasisho, maboresho yoyote ya Programu hii na Huduma unazotumia, ni makubaliano kamili ya Programu hii.

Kwa sababu tunaendelea kutengeneza Programu yetu, tunahitaji kuhifadhi haki, wakati wowote na kwa hiari yetu ya kipekee, kubadilisha masharti ya EULA hii. Tunapofanya hivyo, tutatumia uwezo wetu wote kukuarifu kuhusu tuliyofanya.

 1. SHERIA HUSIKA

Ikiwa kutakuwa na magombano kati yako na sisi, tafadhali tuma barua pepe kwa huduma zetu kwa wateja ili tuweze kujaribu kuyatatua haraka.

EULA hii inadhibitiwa na sheria za Hong Kong bila rufaa kwa migongano yake ya sheria au uchaguzi wa kanuni za sheria. Ikiwa ulinunua Programu hii Marekani, sheria za jimbo unaloishi zinadhibiti madai yote mengine, ikiwa ni pamoja na madai ya sheria za ulinzi wa wateja za jimbo, sheria za madhindano yasiyo sawa, na sheria za uhalifu.

Ufasiri wowote wa EULA hii unafanywa kwa mahitaji ya ndani na ikiwa kutakuwa na mabishano kati ya toleo la lugha ya Kiingereza na lugha yoyote isiyo Kiingereza, toleo la Kiingereza la EULA hii litatawala, kwa kiwango kisichozuiwa na sheria za ndani katika mamlaka yako.

Ikiwa kwa sababu yoyoteile mahakama yenye mamlaka itaona kwamba masharti yoyote, ua sehemu ya masharti, haiwezi kutekelezwa, masharti hayo mengine ya EULA hii yataendelea kutumika kikamilifu.

 1. KANUSHO LA WARANTI

Programu hii na Huduma hizi zinapeanwa kwa leseni kama zilivyo. Unakubali hatari za kuzitumia. KAI haitoi watanti, dhamana au maagizo. Unaweza kuwa na haki za ziada za wateja chini ya sheria zako za ndani ambazo EULA haiwezi kubadilisha. Kwa kiwango kinachokubaliwa na sheria zako za ndani, KAI inatenga waranti za kibiashara na ufaafu kwa madhumuni maalum unaodhaniwa.

 1. VIKWAZO VYA NA UTENGWAJI WA MASULUHISHO NA HASARA

Unaweza kudai hasara za moja kwa moja peke yake hadi bei uliyolipia Programu hii kutoka KAI. Kwa kiwango kinachokubaliwa na sheria zako za ndani, huwezi kudai hasara yoyote nyingine, ikiwa ni pamoja na hasara ya kimatokeo, upungufu wa faida, hasara maalum, isiyo ya moja kwa moja au ya tukio.

 1. Kutumia Huduma kupitia Wavuti

 

KAI inatoa huduma kupitia wavuti na Programu (“Huduma”). Huduma hizi zinaweza kuwa na barua pepe, saa, vikundi vya habari, ukumbi, jamii, kurasa za wavuti za kibinafsi, kalenda, albamu za picha, kabati za wingu, eneo-soko na/au vipengele vinigne vya ujumbe au mawasiliano vilivyoundwa kukuwezesha kuwasiliana na watu wengine. Wakati unatumia Huduma hizi, unakubali kutii sheria husika, EULA hii na kuwa na tabia nzuri. Unakubali kutumia Huduma hizi zote kwa matumizi ya kubinafsi, yasiyo ya kibiashara peke yake na kutuma na kupokea ujumbe na nyenzo zinazofaa na zunazohusiana na Huduma maalum peke yake na baada ya kupokea vibali, ruhusa au leseni zozote zinazohitajika kutuma nyenzo hizo. Unkaubali kuwajibika kwa matokeo yanayoahusiana na nyenzo unazowasilisha. Kama mfano, na sio kikwazo, unakubali kwamba hutatumia Huduma hizi kuchapisha, kupakia na kusambaza barua zozote zisizofaa, barua taka, au nyenzo au taarifa yoyote ya kukashifu, kutukana, isiyo ya kisheria inayoweza kudhuru au kuharibu Huduma hizi au uendeshaji wa kifaa/mali ya mtu mwngine au vinginevyo kukiuka haki za kisheria (kama vile haki za faragha na utangazaji) za watu wengine. Zaidi ya hayo, unakubali kutotuma mifumo yoyote otomatiki au namna za kufikia, kupata, kunakili au kufuatilia sehemu yoyote ya Huduma hizi.

KAI haina wajibu wa kufuatilia Huduma hizi. Hata hivyo, KAI inahifadhi haku ya kufuatilia au kukadiri Huduma hizi, kuhakiki nyenzo zinazochapishwa kwneye Huduma hizi na kuondoa nyenzo zozote kwa hiari yake ya kipekee. KAI inahifadhi haki ya kukatiza au kuzuia ufikiaji wako kwenye Huduma zozote au Huduma zote wakati wowote bila notisi kwa sababu yoyote ile.

KAI inahifadhi haki ya kifochua taarifa yoyote inapoona inafaa ili kutii sheria yoyote husika, kanuni, utaratibu wa kisheria au agozi la serikali, au kuzuia, kukataa kuchapisha au kuondoa taarifa au nyenzo zozote, zikiwa nzima au sehemu yake, kwa hiari ya kipekee ya KAI.