Sisi, KAI OS TECHNOLOGIES (HONG KONG) LIMITED (tukijulikana hapa kama “sisi”, au “Kai”) tunaheshimu wasiwasi wako kuhusu faragha. Sera hii ya Faragha inaeleza sera na taratibu zetu kuhusu taarifa ya kibinafsi na ya aina nyingine kuhusu wateja wetu. Tunakusudia kukupa kiwango fulani cha utulivu na imani kuhusu jinsi tunavyokusanya, kutumia, kufichua, na kulinda taarifa ya kibinafsi na ya aina nyingine tunayokusanya au unayotupatia. Sera hii ya Faragha ya KaiOS (“Sera ya Faragha”) pia inaeleza unavyoweza kuwasiliana nasi ikiwa una maswali au wasiwasi wowote kuhusu taarifa yako ya kibinafsi.

Upeo

Sera hii ya Faragha inaeleza kwa ukamilifu sera yetu na desturi zetu kuhusu ukusanyaji, matumizi na mafichuzi ya taarifa tunayokusanya kupitia tovuti zetu, programu, kurasa za mitandao ya kijamii, ujumbe wa barua pepe, na ununuzi wako au matumizi yako ya bidhaa au huduma zetu, au taarifa ya kibinafsi unayotupatia.

Kwa kutupatia taarifa ya kibinafsi, kufikia tovuti yetu au kuwa kutumia bidhaa au huduma zetu, unakubali kwamba umesoma na kuelewa Sera hii ya Faragha na unakubali sheria na masharti ya Sera hii ya Faragha.

Tutachukua hatua zote busara zinazohitajika kuhakikisha kwamba taarifa yako ya kibinafsi imehifadhiwa na kuchakatwa kwa usalama na kulingana na Sera hii ya Faragha na sheria husika.

Taarifa ya kibinafsi tunayokusanya

Sera hii ya Kibinafsi inatumika kwa taarifa ya kibinafsi, ambayo ni taarifa inayoweza kutumiwa kuwasiliana na au kumtambulisha mtu mmoja.

Tunakusanya taarifa unayotupatia. Tunapokea na kuhifadhi taarifa yoyote kwa usalama unapounda utambulisho wa akaunti, unaponunua bidhaa au huduma zetu, kupakua usasisho wa programu, kuwasiliana nasi au kushiriki katika utafiti wa mtandaoni.

Tunakusanya taarifa ya kiotomatiki. Tunapokea na kuhifadhi aina fulani za taarifa wakati wowote unapowasiliana nasi.

Tunakusanya taarifa inayotumiwa katika mawasiliano yako ya barua pepe na KAI. Ili kutusaidia kufanya baua pepe kuwa muhimu na za kuvutia zaidi, huwa tunapokea udhibitisho mara kwa mara unapofungua barua pepe kutoka kwa tovuti yetu ya ununuzi wa kielektroniki ikiwa kifaa chako kinakubali unweza kama huo. Pia tunalinganisha orodha yetu ya wateja na orodha zinazopokewa kutoka kampuni zingine, ili kuepuka kutuma ujumbe usihitajika kwa wateja wetu.

Tunakusanya taarifa kutoka vyanzo vingine. Tunaweza kupokea taarifa kukuhusu wewe kutoka kwa vyanzo vingine, ulivyoviidhinishwa kuhamisha taarifa kama hiyo kwa washiriki wa tatu na kuiongeza kwenye taarifa yetu ya akaunti.

Tunavyotumia taarifa yako ya kibinafsi

 • Taarifa ya kibinafsi tunayokusanya huturuhusu kukuharifu kuhusu matangazo yetu mapya ya bidhaa, usasisho wa programu, na matukio yajayo. Ikiwahutaki kuwa kwenye orodha yetu ya barua, unaweza kuchaguo kutojumuishwa wakati wowote kwa kusasisha upendeleo wako.
 • Pia huwa tunatumia taarifa yako ya kibinafsi kutusaidia kuunda, kutengeneza, kuendesha, kuwasilisha, na kuboresha bidhaa, huduma, maudhui, na matangazo yetu ili kuboresha tajiriba yako kama mtumiaji kwa uendelevu.
 • Tunaweza kutumia taarifa yako ya kibinafsi kujibu maulizo yako na kutimiza maagizo yako.
 • Tunaweza kutumia taarifa yako ya kibinafsi, ikiwa ni pamoja na tarehe ya kuzaliwa, kuthibitisha utambulisho, kusaidia utambulishaji wa watumiaji, na kuama huduma zinazofaa. Kwa mfano, tunaweza kutumia tarehe ya kuzaliwa kujua umri wa wamiliki wa akaunti za watumiaji.
 • Mara kwa mara, tunaweza kutumia taarifa yako ya kibinafsi kutuma taarifa muhimu, kama vile mawasiliano kuhusu ununuzi na mabadiliko ya sheria, masharti, na sera. Kwa sababu taarifa hii ni muhimu kwa mawasiliano yako nasi, unaweza kuchaguo kutojumuishwa kupokea mawasiliano haya.
 • Pia tunaweza kutumia taarifa yako kibinafsi kwa madhumuni ya ndani kama vile ukaguzi, uchambuzi wa data, na utafiti ili kuboresha bidhaa zetu, huduma, na mawasiliano yetu na wateja.

Ukusanyaji na Matumizi ya Taarifa Isiyo ya Kibinafsi

Pia tunaweza kukusanya taarifa ambayo haihusishwi moja kwa moja na mtu yoyote binafsi. Tunaweza kukusanya, kutumia, kuhamisha na kufichua taarifa isiyo ya kibinafsi kwa madhumuni yoyote. Hii ni baadhi ya mifano ya data isiyo ya kibinafsi tunayoweza kukusanya:

 • Data isiyo ya kibinafsi kama vile lugha, kitambulishi cha kipekee cha kifaa, URL mpendekezaji, eneo, kanda ya saa ambayo bidhaa moja kati ya bidhaa zetu inatumiwa ili tuweze kuelewa tabia ya wateja wetu vizuri na kuboresha bidhaa, huduma, na matangazo yetu.
 • Data isiyo ya kibinafsi kuhusu shughuli za wateja kwenye tovuti yetu, huduma za wingu au duka la programu na kutoka kwa bidhaa na huduma zingine zetu. Taarifa hii inachanganywa na kutumiwa kutusaidia kuboresha taarifa muhimu zaidi kwa wateja wetu na kuelwa sehemu za tovuti, bidhaa, na huduma zetu zinazovutia watu zaidi. Kwa madhumuni ya sera hii ya faragha, aina hii ya data inazingatiwa kuwa taarifa isiyo ya kibinafsi.
 • Maelezo kuhusu unavyotumia huduma zetu, ikiwa ni pamoja na utafutaji, unaoweza kutumiwa kuboresha umuhimu a matokeo yanayotolewa na huduma zetu. Isipokuwa wakati mchache ili kuhakikisha ubora wa huduma zetu kupitia Wavuti, taarifa kama hiyo haitahusishwa na anwani yako ya IP.
 • Kwa kibali chako, tunaweza kukusanya data kuhusu jinsi unavyotumia kifaa na programu zako ili kuwasaidia watengeneza programu kuboresha programu zao.

Ikiwa tutachanganya taarifa isiyo ya kibinafsi na taarifa ya kibinafsi, taarifa inayochanganywa itachukuliwa kama taarifa ya kibinafsi ili mradi isalie ikiwa imechanganywa.

Vidakuzi na Teknolojia Zingine

Tovuti zetu, huduma zetu za mtandaoni, programu wasilianifu, ujumbe wa barua pepe, na matangazo yanaweza kutumia “vidakuzi” na teknolojia zingine. Teknolojia hizi hutusaidia kuelewa tabia ya watumiaji vuzri, kutujulisha sehemu za tovuti watu wanatembelea, na kurahisisha na kupima ufanisi wa matangazo na utafutiaji wa wavuti. Tunachukulia taarifa inayokusanywa na vidakuzi na teknolojia zingine kama taarifa isiyo ya kibinafsi. Hata hivyo, kwa kiwango ambacho anwani za IP au vitambulishi sawa vinazingatiwa kama taarifa ya kibinafsi na sheria za ndani, pia tunachukulia vitambulishi hivi kama taarifa ya kibinafsi. Vile vile, kwa kiwambo ambacho taarifa isiyo ya kibinafsi inachanganywa na taarifa ya kibinafsi, tunachukulia taarifa iliyochanganywa kama taarifa ya kibinafsi kwa madhumuni ya Sera hii ya Faragha.

Kai na wabia watu pia hutuma vidakuzi na teknolijia zingine kukumbuka taarifa ya kibinafsi unapotumia tovuti yetu, huduma zetu za mtandaoni, na programu zetu. Lengo letu katika kesi hizi ni kufanya tajiriba yako na Kai kuwa rahisi na ya kibinafsi zaidi. Kwa mfano, kujua mtu anayetumia kompyuta au kifaa chako amenunua bidhaa fulani au ametumia huduma maalum hutusaidia kufanya matangazo yetu na mawasiliano yetu ya barua pepe kuwa muhimu zaidi kwa matakwa yako.

Unaweza kusanidi kivinjari chako kikubali vidakuzi vyote, kukataa vidakuzi vyote, au kukuarifu wakati kidakuzi kinatumwa. Kila kivinjari ni tofauti, kwa hivyo angalia menyu ya “Msaada” ya kivinjati chako ili ujue jinsi ya kubadilisha upendeleo wako wa vidakuzi.

Katika baadhi ya ujumbe wetu wa barua pepe, tunatumia “URL ya kubofya” iliyounganishwa na maudhui yaliyo kwenye tovuti yetu. Wakati wateja wanabofya mija ya URL hizi, wanapita katika seva tofuati ya wavuti kabla ya kufika ukurasa lengwa wa tovuti yetu. Huwa tunafuatilia data hii ya kubofya ili itusaidie kujua matakwa katika mada fulani na kupia ufanisi wa mawasiliano yetu na wateja. Ikiwa ungependa kutofuatiliwa kwa namna hii, basi hufai kubofya viungo vya maandishi au michoro katika ujumbe huu wa barua pepe.

Huwa Tunashiriki Taarifa?

Huwa hatushiriki taarifa ya kibinafsi na kampuni, mashariki na watu binafsi nje ya Kai isipokuwa moja ya hali zinazofuata zifanyike. Kai inaweza kushiriki taarifa ya kibinafsi kwa kibali chako.

Tunaweza kufichua taarifa ya kibinafsi kwa washiriki wetu inapohitajika ili kutekeleza huduma kwa niaba yetu au yako.

Tunashirikiana na kampuni na watu binafsi kutekeleza shughuli kwa niaba yetu. Mifano inajumuisha kutimiza maagizo, kuwasilisha mizigo, kutuma barua za posta na barua pepe, kuondoa taarifa inayojirudia kutoka orodha ya wateja, kuchanganua data, kutoa usaidizi wa uuzaji, kutoa matokeo na viungo (ikiwa ni pamoja na orodha na viungo vya kulipiwa) vya utafiti, kuchakata malipo ya kadi ya mkopo, na kutoa huduma kwa wateja. Wanaweza kufikia taarifa ya kibinafsi inayohitajika kutekeleza kazi zao, lakini sio kuitumia kwa madhumuni mengine.

Tutashiriki taarifa ya kibinafsi na mashirika au watu binafsi nje ya shirika letu ikiwa tunaamini kwamba ufikiaji, matumizi, uhifadhi au ufichuzi wa taarifa hii unahitajika ili:

 • kutimiza sheria na kanuni zozote husika, utaratibu wa kisheria au maagizo ya kiserikali yanayoweza kutekelezwa.
 • kutambua, kuzuiaau vinginevyo kutatua ulaghai, usalama au matatizo ya kiufundi.
 • kulinda dhidi ya madhara ya haki, mali au usalama wa watumiaji wetu au umma, kama invyohitajika au inavyoruhusiwa na sheria.

Usalama na Uwazi

Tutajitahidi kuchukua hatua na taratibu zote busara halisi, za kiufundi na kishirika ili kulinda taarifa ya kibinafsi tunayokusanya kupitia bidhaa, huduma na tovuti yetu.

Tunafanya kazi kwa bidii kulinda sifa ya kampuni yetu na watumiaji wetu kutokana na ufikiaji usioidhinishwa au ubadilishaji, ufichuzi au uharibifu usioidhinishwa wa taarifa ya kibinafsi tunahifadhi. Hasa:

 • Tunapitia desturi zetu za ukusanyaji, uhifadhi na uchakataji wa taarifa, ikiwa ni pamoja na hatua za usalama halisi, ili kulinda dhidi ya ufikiaji usioidhinishwa kwenye mifumo;
 • Tunaweza kufichamisha inapofaa;
 • Tunatumia ulinzi wa nenosiri inapofaa;
 • Tunaruhusu ufikiaji wa taarifa ya kibinafsi tu kwa wafanyakazi, wakandarasi na wakala wetu wanaohitaji kujua taarifa hiyo ili waichakate kwa niaba yetu na walio katika wajibu wa usiri kutoka na mikataba mikali. Wanaweza kuadhibiwa au mkataba wao unaweza kukatizwa ikiwa watakosa kutimiza wajibu huu.

Hata hivyo, hatua hizi haziondoi wajibu wako wa kuchukua hatua zinazofaa kuweza taarifa yako ya kibinafsi salama, saha kwa kuepuka kutumia utambulisho au manenosiri ya kawaida, kwa kuhakikisha kwamba hufichui nenosiri lako au kumruhusu mtu yoyote mwingine kufikia akaunti yako ya mtumiaji na taarifa yako ya kibinafsi, na hatua zozote zingine za ulinzi zinazotumika.

Kuhusu uwazi, lengo letu ni kuwa wazi kuhusu taarifa tunayokusanya, ili uweza kufanya uamuzi kuhusu jinsi inatumiwa.

Ukishiriki taarifa yako ya kibinafsi kupitia moja ya tovuti, huduma au bidhaa zetu na akaunti ya mshiriki wa tatu, kama vile Facebook, Google+ au Twitter, tafadhali jua kwamba fara ya taarifa yako ya kibinafsi itadhibitiwa na mtawalia na mmoja wa washiriki hawa watatu. Hatuwajibiki kwa uharibifu wowote unaotokana kwa sababu ya upoteaji, uharibifu au matumizi yoyote mabaya ya data yanayoweza kutokea kwenye wasifu wako wa mshiriki wa tatu ambao huwezi kuudhibiti.

Taarifa yoyote ya kibinafsi au maudhui iliyofichua kwa hiari yako ukitumia tovuti, huduma au bidhaa zetu na yanayoweza kutazamwa na watumiaji wa programu au tovuti za mshiriki wa tatu (kama vile maeneo ya sogoa, katika ujumbe) huweza kutazamwa na umma na yanaweza kukusanywa, kutazamwa na kutumiwa na watu wengine. Una wajibu wa taarif ayako kibinafsi unayochagua kushiriki au kuwasilisha.

Watoto

Tunaelewa umuhimu wa kuchukua hatua zaidi za tahadhari ili kulinda faragha na usalama wa watutu wanaotumia bidhaa na huduma zetu. Kwa hivyo, huwa hatukisanyi, kutumia au kufichua taarifa ya kibinafsi kutoka kwa watoto wenye umri chini ya miaka 13, au umri sawa wa chini katika mamlaka husika tukijua, bia kibali cha mzazi kinachoweza kuthibitishwa. Tukifahamu kwamba tumekusanya taarifa ya kibinafsi ya mtoto mwenye umri wa chini ya miaka 13, au umri sawa wa chini kulingana na mamlaka, bila kupokea kibali cha mzazi kinachoweza kuthibitishwa tutachukua hatua ya kufuta taarifa hiyo haraka iwezekanavyo.

Mabadiliko

Sera yetu ya Faragha inaweza kubadilishwa mara kwa mara. Tutachapisha mabdiliko yoyote ya Sera ya Faragha kwenye ukurasa ya tovuti na, ikiwa mabadiliko ni makubwa, tutatoa notisi bora zaidi (inayojumuisha, kwa huduma fulani, taarifa ya barua pepe ya mabadiliko ya Sera ya Faragha). Pia tutadumilisha matoleo ya awali ya Sera hii ya Faragha katika jalada kwa mapitio yako.

Toleo la sasa ni la tarehe 30 Juni, 2017.

Udumishaji wa Taarifa ya Kibinafsi

Huwa tunahifadhi taarifa yako ya kibinafsi kwa muda mfupi unaohitajika kutimiza madhumuni yaliyoorodheshwa katika Sera hii ya Faragha isipokuwa muda mrefu ua udumishaji unahitajia au kuruhusiwa na sheria na kwa madhumuni yaliyofafanuliwa hapa juu. Baada ya madhumuni haya kutumizwa, taarifa yote ya kibinafsi inafutwa kwa mbinu salama.

Huduma Zinazotegemea Eneo

Ili kutoa huduma zinazotegemea eneo zilizo kwenye bidhaa zetu au za wabia wetu, Kai na wabia wetu na washiriki waliopewa leseni wanaweza kukusanya, kutumia, na kushiriki data ya eneo mahsusi, ikiwa ni pamoja eneo la muda halisi la kijiografia la kifaa chako. Inapotumika, huduma zinazotegemea eneo zinaweza kutumia GPS, Bluetooth, na anwani yako ya IP, pamoja na maeneo ya Wi-Fi ya umma na maeneo ya minara ya simu, na teknolojia zingine ili kujua eneo la kifaa chako. Isipokuwa umetoa kibali, data hii ya eneo inakusanywa bila vitambulishi kwa namba ambayo haikutambilishi kibianfsi na inatumiwa na Kai na wabia wetu na washiriki wenye leseni kutoa na kuboresha bidhaa na huduma zinazotegemea eneo. Kwa mfano, kifaa chako kinaweza kushiriki eneo lake la kijiografia na watoa programu unapochagua kujiunga katika huduma zao za eneo.

Tovuti na Huduma za Washiriki wa Tatu

Tovuti. Bidhaa, programu, na huduma za Kai zinaweza kuwa na viungo vya tovuti, bidhaa, na huduma za washiriki wa tatu. Bidhaa na huduma za Kai pia zinaweza kutumia au kutoa bidhaa au huduma kutoka washiriki wa tatu. Taarifa inayokusanywa na washiriki wa tatu inayoweza kujumuisha mambo kama vile data ya eneo au maelezo ya anwani, inadhibitiwa na desturi za faragha. Tunapendekeza ujifunze kuhusu desturi za faragha za washiriki hao wa tatu.

Haki zako: Ufikiaji, Uhariri, Uzuiaji

Unaweza kufikia, kupitia na kuhariri taarifa yako ya kibinafsi wakati wowote kwa kuingia kwenye akaunti yako ya mtumiaji, kutembelea wasifu wako wa mtumiaji au kwa kuwasiliana nasi moja kwa moja. Ikiwa utahitaji tuhariri au tufute taarifa yako ya kibinafsi, tunaweza kukuomba utupatie ushahidi wa utambulisho wako kabla tuchukue hatua kutekeleza agizo lako.

Pia unaweza kuomba data yako ifutwe au izuiwe, inapofaa, ikiwa unaamini kwamba data yako sio sahihi.

Kwa maagizo yoyote kama yaliyofafanuliwa hapa juu, unaweza kutumia agizo lako kwa anwani ya barua pepe inayofuata: privacy@kaiostech.com

Katika mamlaka fulani na sheria zingine za ulinzi wa data, unaweza kuwa na haki ya kuagiza maelezo ya taarifa yako ya kibinafsi tunayoihifadhi inayokuhusu au kuagiza usahihishaji au ufutaji wa taarifa yako ya kibinafsi.

Tafadhali tusaidie kuhakikisha kwamba taarifa yako kibinafsi tunayoihifadhi kukuhusu ni sahihi na iliyosasishwa. Ikiwa unafikiria kwamba taarifa yoyote ya kibianfsi tuliyoihifadhi kukuhusu sio sahihi au kamili, tafadhali wasiliana nasi kupitia privacy@kaiostech.com.

Maswali ya Faragha

Ikiwa una maswali au wasiwasi wowote kuhusu Sera ya Faragha au uchakataji wa data, au ukuwa ungependa kutoa malalamiko kuhusu ukiukaji wa sheria za faragha za ndani unaoshuku, tafadhali wasiliana nasi. Ubaweza kuwasiliana nasi kwa kutuma barua pepe kwa privacy@kaiostech.com.

Mawasiliano yote yanakaguliwa na kujibiwa haraka iwezekanavyo. Ikiwa hujaridhishwa na jibu ulilopokea, unaweza kutuma malalamiko yako kwa mdhibiti husika katika mamlaka yako. Ukituagiza, tutajitahidi kukupatia taarifa kuhusu njia muhimu za kutuma malalamiko zinazoweza kutumika katika hali yako.